Je, Mungu alimuumba Shetani?
Shetani ni nani? Wengi huamini kuwa shetani ni kiumbe flani wa kufikirika, lakini Biblia inasema kuwa shetani ni halisi, na amenuia kukudanganya wewe na kuharibu maisha yako, ukweli ni kwamba kiumbe huyu ni mwenye akili na katili tofauti na ulivyoambiwa apo awali, anateka mtu mmoja mmoja, familia, makanisa na hata mataifa yote akiongeza huzuni na maumivu katika ulimwengu huu, zifuatazo ni kweli za Biblia kuhusu huyu mfalme wa giza na namna unavyoweza kumshinda 1. Ni nani aliye mwanzilishi wa dhambi? “atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo” 1 Yohana 3:8. “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye” Ufunuo 12:9 Jibu: Shetani ambaye pia huitwa ibilisi ndiye muanzilishi wa dhambi, Bila biblia asili ya dhambi ingebaki kuwa siri. 2. Shetani aliitwa nani kabla ya kufanya dhambi? Alikuwa akiishi wapi? “Jinsi ulivyoang...
Comments
Post a Comment