Je, Mungu alimuumba Shetani?
Shetani ni nani? Wengi huamini kuwa shetani ni kiumbe flani wa kufikirika, lakini Biblia inasema kuwa shetani ni halisi, na amenuia kukudanganya wewe na kuharibu maisha yako, ukweli ni kwamba kiumbe huyu ni mwenye akili na katili tofauti na ulivyoambiwa apo awali, anateka mtu mmoja mmoja, familia, makanisa na hata mataifa yote akiongeza huzuni na maumivu katika ulimwengu huu, zifuatazo ni kweli za Biblia kuhusu huyu mfalme wa giza na namna unavyoweza kumshinda
1. Ni nani aliye mwanzilishi wa dhambi?
“atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo” 1 Yohana 3:8.
“Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye” Ufunuo 12:9
Jibu: Shetani ambaye pia huitwa ibilisi ndiye muanzilishi wa dhambi, Bila biblia asili ya dhambi ingebaki kuwa siri.
2. Shetani aliitwa nani kabla ya kufanya dhambi? Alikuwa akiishi wapi?
“Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa” Isaya 14:12
“Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme” Luka 10:18
“Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto” Ezekiel 28:14.
Jibu: shetani alikuwa akiitwa nyota ya alfajiri(lusifa), na alikuwa akiishi mbinguni
3. Nini ilikuwa asili ya shetani? Biblia inamuelezeaje?
“Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari. Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako” Ezekiel 28:12-15
Jibu: lusifa aliumbwa na Mungu, kama malaika wengine walivyoumbwa (waefeso 3:9) lusifa alikuwa ni kerubi afunikaye au malaika. Moja ya kerubi afunikaye alikuwa akisimama upande wa kushoto wa kiti cha enzi cha Mungu na mwingine upande wa kulia (zaburi 99:1) lusifa likuwa mmoja wa malaika wa ngazi ya juu alikuwa ni kiongozi, uzuri wake ulikuwa usio na dosari na wenye kushangaza, hekima yake ilikuwa kamilifu, akiwa na mng’ao angavu wenye kushangaza. Zekiel 28:13 inaelezea ya kuwa aliumbwa kuwa mwanamuziki wa aina yake, baadhi ya wasomi wa maandiko wanaamini alikuwa ni kiongozi wa kwaya ya malaika.
4. Nini kilitokea katika maisha ya lusifa hata akafanya dhambi? Je, lusifa alifanya dhambi gani?
“Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya
mwangaza wako” Ezekiel 28:17
“Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu” Isaya 14:13-14.
Jibu: kiburi, wivu, na kutotosheka kuliinuka katika moyo wa lusifa, muda si mrefu akaanza kutamani naafasi ya Mungu na kumtaka kila mmoja amuabudu yeye.
Zingatia: kwanini ibada ni kitu muhimu sana? Ndiyo sababu has ya pambanio linaloendelea kati ya Mungu na Shetani, watu waliumbwa wawe na furaha na wanaojitosheleza kwa kumuabudu Mungu tu. Wala si viumbe wa mbiguni yaani malaika wanaostahili kuabudiwa (ufunuo 22:8,9) karne moja baadae alipo mjaribu yesu pale jangwani bado alikuwa katika harakati za kutaka kuabudiwa tu, na ndiyo lilikuwa jaribu kuu (mathayo 4:8-11) sasa, katika hizi siku za mwishi Mungu anaita watu wote wamuabudu yeye(ufunuo 14:6,7) jambpo hili linamchnganya na kumkera sana shetani hata atajaribu kuwalazimisha watu wamuabudu yeye au la sivyo wauawe (ufunuo 13:15) kila mtu naabudu kitu Fulani: madaraka, ufahari, chakula, starehe, mali, nk. Lakini Mungu anasema “usiwe na miungu mingine ila mimi” (Kutoka 20:3) kama lusifa, tunao uhuru a kuamua juu ya nani tumuabudu, endapo tutaamua kuabudu kitu kingine cchote au mtu mwingine yoyote zaidi ya Muunbaji wetu, ataheshimu maamuzi yetu lakini tutahesabiwa kuwa kinyume chake (mathayo 12:30) kama kitu chochite au mtu yoyote zaidi ya Mungu anachukua naafasi ya kwanza katika maisha yetu, tutaishia kufuata hatua za shetan, je Mungu ana naafasi ya kwanza katika maisha yako?
5. Nini kilitokea mbinguni kama matokeo ya dhambi ya lusifa?
“Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake, 8. nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye” Ufunuo 12:7-9.
Jibu: lusifa aliadanganya theluthi ya malaika (ufunuo 12:3,4) na kusababisha uasi mbinguni, Mungu hakuwa na chaguo linginze zaidi ya kumtupa shetani na malaika wengine waasi, kwasababu lengo la lusifa ilikuwa ni kuchuka naafasi ya Mungu katika kiti chake, hata kama jambo hilo lingehusisha uuaji (Yohana 8:44) baada ya kufukuzw toka mbinguni, lusifa akaitwa shetani, ikiwa na maana “aliye kinyume cha” na ibilisi ikimaanisha “muasi” na malaika waliomfuata shetani wakaita mapepo/majini.
6. Makao makuu ya shetani yako wapi? Je anajisikiaje kuhusu jamii ya wanadamu?
“Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi? Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo” Ayubu 2:2
“Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana Yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu” Ufunuo 12:12.
“Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzungukazunguka, akitafuta mtu ammeze” 1 Petro 5:8.
Jibu: tofauti na imani iliyoenea sana, makao makuu ya shetani ni duniani, na siku kuzimu kama wengie wananyo amini, Mungu alimpa Adam na Eva utawala wa dunia (mwanzo 1:26) walipofanya dhambi, wakapoteza utawala huu kwa shetani (Warumi 6:16), ambaye sasa akwa mtawala,au mfalme wa dunia (Yohana 12:31). Shetani anawachukia wanadamu, abao wameumbwa kwa mfano wa Mungu, kwasababu hawezi kumdhuru Mungu moja kwa moja, anaelekeza hasira yake kwa watoto wa Mungu waliopo duniani, ni mmujai mwenye chuki kubwa ambaye lengo lake ni kukuharibu wewe, na kuumiza Mungu.

good scripts
ReplyDeleteAmina barikiwa Mungu atutie nguvu maana anatuchonganisha na Mungu mumbaji wetu kwhy anahasira sana na sisi
ReplyDelete