MAMBO HAYO YATAKUWA LINI? NAYO NI NINI DALILI YAKUJA KWAKO?
Wanafunzi wa Yesu kama sisi leo, walikuwa na shauku ya kujua, ni lini mambo yatabadilika? ni lini magonjwa, vifo, vilio, dhuruma, ukatili, usaliti, na uovu vitakoma? ni lini haki ya kweli itapatikana? ni lini fedhea ambayo imetawala mioyo yao ingeondoka? wakakumbuka ahadi ya Yesu aliyoisema
Na ndipo wakauliza, t"Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? Mathayo 24:3
Ndipo Yesu anatoa ufafanuzi kuhusu ujio wake mara ya pili
1. HAKUNA AJUAYE SIKU WALA SAA YA KUJA KWAKE.
Yesu anasema "Kesheni basi, kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu, Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. Mathayo 24:42-43
"Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa." Mathayo 25:13
"Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu." Luka 12:40
2. DALILI ZA KUJA KWA YESU.
Tumeona kuwa hakuna ajuaye siku wala saa ya kuja kwa Yesu, lakini akawaambia dalili (viashiria), ya kwamba kwa kuona mambo haya yakitokea mjue ya kuwa kurudi kwangu kumekaribia
WALIMU WA DINI WA UONGO
“Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye.
Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi” Mathayo 24:4,5,6
“Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi” Mathayo 24:11.
“Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule” Mathayo 24:24
Zingatia maneno haya makristo wa uongo, manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu wapate kuwapoteza, kama ya mkini hata walio wateule, maandiko haya leo yametimia kwa kuchipuka kwa manabii, mitume, na viongozi wengi wa kidini ambao wamefungua nyumba za ibada, na sasa inakuwa ni vigumu kutambua yupi mkweli na yupi muongo, zingatia huduma zao zimejawa na matendo ya miujuza sawa sawa na yesu alivyosema miujiza ambayo imelenga kuwapoteza wengi wamuache Mungu wa kweli
MAMBO YA KUZINGATIA
- MIUJIZA SI KIGEZO CHA KUWA MTU HUYO ANA MUNGU WA KWELI Yesu anasema “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu” Mathayo 7:22,23.
- TUWAPIME KWA MAANDIKO MATAKATIFU “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao, hapana asubuhi”. Isaya 8:20 “Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua” Mathayo 7:16-20.
kwanini walimu wa dini wa uongo wanatokea? shetani anajua ya kuwa ana muda mchache sana wa kuendelea kuudanganya ulimwengu ili ajikusanyie kundi kubwa la kuangamia nalo na kwa hiyo anatumia njia ya dini kuingiza madanganyo yake kwa watu wengi, kama Yesu alivyompinga mjaribu sisi nasi tunatakiwa kusema "imeandikwa" Mathayo 4:4-7
Comments
Post a Comment