Posts

Je, Mungu alimuumba Shetani?

Image
Shetani ni nani? Wengi huamini kuwa shetani ni kiumbe flani wa kufikirika, lakini Biblia inasema kuwa shetani ni halisi, na amenuia kukudanganya wewe na kuharibu maisha yako, ukweli ni kwamba kiumbe huyu ni mwenye akili na katili tofauti na ulivyoambiwa apo awali, anateka mtu mmoja mmoja, familia, makanisa na hata mataifa yote akiongeza huzuni na maumivu katika ulimwengu huu, zifuatazo ni kweli za Biblia kuhusu huyu mfalme wa giza na namna unavyoweza kumshinda 1. Ni nani aliye mwanzilishi wa dhambi? “atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo” 1 Yohana 3:8. “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye” Ufunuo 12:9 Jibu: Shetani ambaye pia huitwa ibilisi ndiye muanzilishi wa dhambi, Bila biblia asili ya dhambi ingebaki kuwa siri. 2. Shetani aliitwa nani kabla ya kufanya dhambi? Alikuwa akiishi wapi? “Jinsi ulivyoang...
MAMBO HAYO YATAKUWA LINI? NAYO NI NINI DALILI YAKUJA KWAKO? Wanafunzi wa  Yesu kama sisi leo, walikuwa na shauku ya kujua, ni lini mambo yatabadilika? ni lini magonjwa, vifo, vilio, dhuruma, ukatili, usaliti, na uovu vitakoma? ni lini haki ya kweli itapatikana? ni lini fedhea ambayo imetawala mioyo yao ingeondoka? wakakumbuka ahadi ya Yesu aliyoisema "Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo" Yohana 14:1-3 Na ndipo wakauliza, t "Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? Mathayo 24:3 Ndipo Yesu anatoa ufafanuzi kuhusu ujio wake mara ya pili 1. HAKUNA AJUAYE SIKU WALA SAA Y...